
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako.
Profesa Joyce Ndalichako, ameyasema hayo jijini Dodoma kwenye maonyesha ya MAKISATU ambayo yamewakusanya wabunifu mbalimbali na kuwataka vijana kukubaliana na mabadiliko ya teknolojia ambayo kwa siku za hivi karibuni yamechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo Duniani.
"Nitoe wito kwa vijana katika taasisi za elimu ya juu wale ambao wana ubunifu, wasisite kuonesha ubunifu wao na serikali itaendelea kuwawekea mazingira wezeshi ili waweze kuendeleza ubunifu wao", amesema Waziri Ndalichako