Wednesday , 5th May , 2021

Maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu wa nchini England tayari wamejiandaa kumiminika kwenda jijini Istanbul kuangalia mchezo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani ulaya na tiketi elfu 8 kutolewa kwa mashabiki wa Man City na Chelsea.

Baadhi ya Mashabiki wa Manchester City (kulia) wakionekana kusheherekea baada ya timu hiyo kutinga fainali kwa mara ya kwanza ya UEFA.

Shirikisho la soka barani ulaya UEFA limekataa kuhamisha mchezo wa fainali kutoka Uturuki kwenda Wembley kwasababu uturuki iko kwenye zuio la COVID 19 la kutoshiriki mikutano.

Manchester City na wapinzani wao katika fainali ya Ligi ya Mabingwa watapokea tiketi Elfu 4, kila timu, huku UEFA na mamlaka za Uturuki wanaaminika wanaweza kuandaa mipango ya kuchukua watazamaji elfu 25 kwenye Uwanja wa Ataturk kwa mechi hiyo ya fainali Mei 29.

Ikiwa imeidhinishwa kwamba uwanja wa Istanbul utachukua theluthi moja ya uwezo wake wa kuchukua mashabiki elfu 76, Lakini kuruhusu mashabiki kwenye mchezo huo itakua ni kufanyia mzaha zuio la covid 19.

Mamlaka zinadai ni kwenda kinyume na wataalam wa afya ya umma, Hivyo mashabiki wa England hawapaswi kuruhusiwa kuhudhuria mchezo huo kwa sababu ya kiwango cha juu cha maambukizi ya virusi vya corona nchini Uturu.