Wednesday , 5th May , 2021

Ni ushindi mwingine kwa Burna Boy, mshindi wa tuzo ya Grammy kama ilivyo kwa wimbo wake “Ye” wa mwaka 2018, baada ya kupokea udhibitisho kuwa wimbo huu umefikia mauzo ya dhahabu (Gold) kutoka The Recording Industry Association of America (RIAA)

Msanii Burna Boy

Wimbo huo una miaka mitatu tangu umeachiwa na unapatikana kwenye album ya sita “outside” na umefanikiwa kuuza zaidi ya nakala 500,000.

2019 Burna boy alishinda tuzo ya wimbo bora wa mwaka na chaguo la msikilizaji kwenye Soundcity MVP Awards Festival na The Headies kupitia wimbo huu huu wa “Ye”.