Wednesday , 5th May , 2021

Shirikisho la soka Africa kusini 'SAFA' limemtangaza raia wa Ubelgiji Hugo Broos kuwa kocha mpya wa Bafana Bafana.

Kocha Hugo Broos

Broos anachukua nafasi iliyoachwa wazi na kocha mzawa Molafi Ntseki aliyetimuliwa na shirikisho hilo mwezi Machi mwaka huu, baada ya kushindwa kufuzu AFCON kwa mwaka 2022 nchini Cameroon.

Michuano ya AFCON 2021 ililazimika kusogezwa mbele hadi mwaka 2022 kufuatia janga la Corona lililoikumba dunia na kulazikika kuchezwa mwaka huo kuanzia Januari 6 hadi Februari 9 ambayo ndiyo itahitimishwa.

Hugo Broos mwenye umri wa miaka 69 ni kocha mzoefu katika soka la Africa, akifundisha katika ngazi ya vilabu na timu za taifa kwa zaidi ya miaka 7, alianza na klabu ya JS Kabylie ya Algeria na baadaye timu ya taifa ya Cameroon ' The Indomitable Lions'

Ni kocha mshindi wa AFCON mwaka 2017 akiwa na kikosi cha Cameroon kisicho kuwa na nyota kadhaa waliokataa kuungana naye akiwemo Joe Matip wa liverpoo, wadau wengi wa likosa kukiamini kabisa, lakini walifanikiwa kutwaa baada ya kuifunga Misri 2-1 katika fainali hiyo.

Awali makocha kadhaa walikuwa wanapewa upatu mkubwa kuchukua nafasi hiyo akiwemo Benedict Mc Carthy ambaye ni nyota wao wa zamani anayeshikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote akiwa na goli 31, Pitso Mosimane anayefundisha Al Ahly alipewa nafasi kubwa sana lakini mwisho wa siku ni Hugo Broos.