
Mwenyekiti wa watoa huduma ya Mafuta na Gesi nchini Abdulsamad Abdulrahim
Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei, 5, 2021, kupitia kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, ikiwa ni miongoni mwa wafanyabiashara walioongozana na ujumbe wa Rais Samia Suluhu Hassan, katika ziara yake ya kikazi nchini Kenya ambayo aliianza jana.
"Katika maeneo ya ufugaji Watanzania tusilalamike kwamba hatupewi fursa, fursa zipo zinakuja lakini je tuna vigezo, siyo unaambiwa leta Kuku 1,500 wa kienyeji halafu unaleta Kuku 200 halafu 1,000 unawapachika wale wa kutoka nje vitu hivi havitakiwi, tubadilike, tuwe wakweli", amesema Abdulsamad
Aidha ameongeza kuwa, "Nitoe wito kwa Watanzania wenzangu, viongozi wa nchi wanafanya wajibu wao, sisi imefika wakati wa kushirikiana na ndugu zetu Wakenya katika kuangalia ule mnyororo wa thamani nini tunaweza kufanya ama kushirikiana nao".