
Naibu Wazxiri, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi
Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 4, 2021, jijini Dodoma wakati akijibu maswali ya mbunge wa Mlalo, Abdallah Shangazi, kuhusu uwepo wa rushwa katika sekta ya michezo, huku akiongeza kuwa licha ya kuchukua hatua mbalimbali ya kuziba mianya rushwa bado pia wataendelea kuwachukulia hatua watuhumiwa wote wa rushwa katika sekta hiyo.
"Ili kuziba mianya ya rushwa niwaase TFF na timu za mpira wa miguu waachane na tiketi zile za kuchana na waweze kwenda kwenye 'electronic ticket' hii itasaidia sana upungufu na upotevu wa mapatao, itaongeza mapato kwa timu zao lakini vilevile kwa TFF", amesema Ndejembi
Aidha ameongeza kuwa "Imeonekana kuwa ikiwa timu ya Simba inacheza uwanja unajaa sana, lakini bado mapato yanakuwa ni hafifu ukilinganisha na timu nyingine ambayo ni kubwa Afrika Mashariki na kati"