Saturday , 1st May , 2021

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Hispania La Liga Real Madrid wataendelea kumkosa nahodha wa kikosi hicho Sergio Ramos kwenye mchezo wa usiku wa leo wa ligi kuu dhidi ya Osasuna.

Sergio Ramos

Ramos anasumbuliwa na majeruhi na hajacheza toka Machi 13 mwaka huu, mlinzi huyo anasumbuliwa na majeraha ya misuli ambayo yamemfanya akose michezo kadhaa ikiwemo michezo ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Liverpool na mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali dhidi ya Chelsea ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Ramos alifanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha Los Blancos siku ya Alhamis na Ijumaa, lakini inaripotiwa kuwa kocha wa kikosi hicho Mfaransa Zinedine Zidane ameamua kutomtumia kwenye mchezo wa leo dhidi ya Osasuna, akiwa na hofu huwenda akaumia tena na kaukosa mchezo wa marejeano dhidi ya Chelsea siku ya Jamatano Mei 5, 2021.

Kocha Zidane pia atakosa huduma za wachezaji Ferland Mendy mwenye majeruhi na Fede Valverde ambaye alikutwa na maambukizi ya Corona lakini wachezaji Dani Carvajal na Lucas Vazquez wao ni majeruhi wa muda mrefu na watakosa michezo yote iliyosalia ya msimu huu.

Real Madrid inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa La Liga ikiwa na alama 71 tofauti ya alama mbili na vinara Atletico Madrid wenye alama 72, na Osasuna wapo nafasi ya 11 wakiwa na alama 40.