Saturday , 1st May , 2021

Mcheza kikapu nyota wa timu ya Los Angeles Lakers, Lebron James amerejea dimbani kwa mara ya kwanza tokea Marchi 30, 2021 alfajiri ya kuamkia leo kwenye mchezo wa ligi ya kikapu nchini Marekani na kupoteZa kwa alama 110 kwa 106 dhidi ya Sacramento Kings.

Lebron James wa LA Lakers (wakwanza kushoto) wakijaribu kuwatoka walinzi wa Sacramento Kings usiku wa kuamkia leo kwenye NBA.

Lebron alipata majeraha ya kifundo cha mguu na kumfanya awe nje kwa muda mrefu zaidi kwa mara ya kwanza kwenye NBA na kuipiku rekodi ya kuwa nje kwa michezo 18 msimu wa mwaka 2018-2019.

Baada ya kurejea, Lebron alicheza kwa dakika 28 na kufanikiwa kuisaidia timu yake la Lakers ambao ndiyo mabingwa watetzi wa NBA kwa kupata alama 16, rebaundi 8 na kutengeza magoli 7 ambayo hayakutosha kuwapa ushindi na kubadilisha upepo mbaya wa matokeo.

Kurejea kwake ni taarifa njema wa kocha wake Frank Vigel ambaye amesema, “Ni muda wa kurejea kwa Lebron na tunafuraha sana. Hakuna mipak aya dakika ya yeye kucheza”.

Takwimu zinaonesha kuwa tokea Lebron akosekane, Lakers walicheza michezo 20, wakipata ushindi michezo 8 pekee huku wakipata vipigo kwenye michezo 12 vikiwemo vipigo vitatu mfululizo kwenye vipigo vine mfululizo kwenye michezo yao mitano ya mwisho.

Wakati ikiwa imesalia michezo 10 kwa Lakers kudhihirisha matumaini yao ya kutetea taji lao la NBA, huenda mashabiki na timu hiyo waka na furaha kwani Lebron James pamoja na Anthony Davis wamereja dimbani kwa pamoja jambo linalowafanya warudi kwenye kiwango bora.

Kwasasa, Lakers inashika nafasi ya 5 kwenye msimamo wa NBA kwa upande wa Mashariki wakilenga kumaliza kwenye nafasi hizo ili kucheza michezo ya mtoano kuelekea fainali ya NBA msimu huu.

NBA itaendelea tena usiku wa kuamkia kesho kwa michezo 11, vinara wa Mashariki, Utah Jazz watakipiga dhidi ya Toronto Raptors saa 11:00 Alfajiri, Dallas Mavericks watacheza na Washington Wizards ilhali Los Angeles Clippers na Denver Nuggets watacheza saa 11 Alfajiri.