
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Maadhimisho hayo kitaifa yanafanyika mkoani Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Tayari viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba, Waziri wa Afya Doroth Gwajima, Waziri wa Nchi, Sera,Bunge,ajira,vijana na wenye ulemavu Jenista Mhagama wameshawasili uwanjani.
Viongozi wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara Habari Dkt. Hassan Abbasi ambaye naye tayari yupo kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mh. Shanif Mansoor, akiwa pamoja na wabunge wengine naye yupo kwenye uwanja wa CCM Kirumba.