Friday , 30th Apr , 2021

Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini leo imewafikisha mahakamani raia saba wa Iran kwa kosa la uhujumu uchumi, mara baada ya kukamatwa na dawa za kulevya kilo 859.08  zilizokuwa zimefichwa ndani ya Jahazi lililokuwa likitokea Nchini mwao. 

Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za Kulevya, Kamishna Jenerali Gerald Kusaya akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.

Kamishina Jenerali wa Mamlaka hiyo Gerald Kusaya akizungumza  na waandishi wa habari amesema Kesi Waliosomewa  watuhumiwa hao ni ya mashtaka ya kusafirisha madawa ya kulevya namba 02 ya mwaka 2021 mbele ya hakimu mkazi Mfawidhi Maria Bantulayne.

Kati hatua nyingine Kusaya ametaja madhara yanayosababishwa na matumizi ya madawa ya kulevya kuwa ni Magonjwa ya Moyo, Sukari, Ini, Figo pamoja na Afya ya akili.

Dawa za kulevya ndio chanzo cha kupoteza nguvu kazi ya Taifa, inasababisha magonjwa hatarishi ikiwepo Ugonjwa wa Akili, Moyo, Ini, Figo lakini pia inasababisha ongezeko la Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI “, amesema Kusaya.

Ukamataji huo utanatajwa kuwa mkubwa kufanyika nchini tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo mwezi Februari 2017.