
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Christina Mndeme
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho kupitia kwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole imeeleza kuwa Mndeme amepitishwa na Halmashauri Kuu Taifa ya Chama hicho baada ya kupendekezwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Samia Suluhu Hassan.
Mndeme anachukua nafasi iliyokuwa inashikwa na Lodrick Mpogolo, ambaye atapangiwa majukumu mengine.