
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongoro
Chongoro amependekezwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Samia Suluhu Hassan kisha Halmashauri Kuu Taifa ya Chama hicho kumpitisha, katika kikao chake cha leo jijini Dodoma.
Chongoro anachukua nafasi ya Dkt. Bashiru Ally aliyeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.