Thursday , 29th Apr , 2021

Winga wa zamani wa Chelsea Damien Duff amemponda Eden Hazard kwa kusema kwamba Hazard Hajawahi kuwa na kiwango cha hali ya juu kama Messi na Ronaldo. Duff ameongeza kusema winga huyo wa Real Madrid anaweza asirudi tena kwenye kiwango chake bora kwani sasa ame nenepa sana tofauti na zamani

Winga wa zamani wa Chelsea, Darmian Durf (kushoto) na Eden Hazard (kulia).

 

Duff amekosoa mwenendo wa Eden Hazard tangu alipohamia Real Madrid mwaka 2019, akisema kuwa kamwe hawezi kulinganishwa na Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kwa sababu hajawahi kuwa na kiwango bora cha hali ya juu duniani.

Maneno hayo mazito aliyasema baada ya mchezo wa sare ya bao 1-1 wa mchezo wa nusu fainali ligi ya mabingwa ulaya Jumanne usiku Madrid chidi ya Chelsea ambao ulikuwa ni mchezo wa 16 kwa Hazard akiwa na Los Blancos msimu huu.

Duff ambaye aliwahi kucheza misimu mitatu Chelsea na kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu, anaamini kwamba Hazard amekuwa akipambana sana na uzito wake kila wakati, na anapaswa kuweka bidii zaidi aweze kukaa sawa.

Eden Hazard alihamia Real Madrid kutoka Chelsea mwaka 2019 kwa dau la paund milioni 130 na amekua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara kitendo ambacho kimemfanya kucheza michezo michache.