
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akikabidhi zawadi kwa ajili ya Wazee na watoto wanaolelewa katika makazi ya 'Maria Theresa House' Mburahati, Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Jingu ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam alipotembelea makazi ya Watoto na Wazee wasiojiweza ya Mama theresa yaliyoko Mburahati.
Amesema Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambayo ina dhamana na Wazee na watoto itahakikisha inatekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia taifa kupitia Bunge jijini Dodoma.
“Mimi ndio mtumishi Mkuu kwenye eneo hili na kazi yangu kubwa ni kuhakikisha kwamba maelekezo ya Rais aliyoyatoa wakati akihutubia taifa Bungeni hivi karibuni, yanatekelezwa kwa kasi kubwa”amesema Dkt. Jingu
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Flora Emmanuel ameeleza kufarijika kutokana na hatua zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya sita kwa kuhakikisha walengwa hao wanaishi katika mazingira bora.
“umetuletea ujumbe mzuri,sio kwetu sisi tu humu ndani bali hata nje. Mwenyezi Mungu akupe baraka na nguvu ya kufanya kazi,” amesema Flora.
Akihutubia Taifa kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 22, mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan aliweka bayana vipaumbele vya Serikali katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma kwa makundi maalum zikiwemo huduma kwa watoto na Wazee wasiojiweza.