Wednesday , 19th Nov , 2014

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii nchini Tanzania imesema kupitia mpango wa matokeo makubwa sasa BRN imetoa vipaumbele vinne ambavyo vitasaidia katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini.

Katibu mkuu wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donald Mbando.

Katibu mkuu wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donald Mbando amesema moja ya vipaombele hivyo ni kuhakikisha inaongeza rasilimali watu katika sekta hiyo na imetangaza kuongeza udahili wa wanafunzi vyuoni ambapo hadi kufikia mwaka 2017 itakuwa imedahili wanafunzi vuoni wapatao elfu 10.

Dkt. Mbando amesema mpaka sasa wameshadahili wanafunzi elfu 8 hivyo pia kuna uwezekano mkubwa wa kuvuka malengo yaliyokusudiwa na chini ya mpango huo serikali itahakikisha inapunguza changamoto katika sekta hiyo.

Aidha Dkt. Mbando amesema kuwa idadi ya Wanafunzi itakayoongeza inaweza kumaliza matatioz yanayojitokeza sasa ya baadhi ya Zahanati au vituo vya Afya kukosa wauguzi.