Saturday , 13th Feb , 2021

The African Princess Nandy amefunguka kusema mpenzi wake Billnass amemwambia anataka kuwa na watoto 6 kutoka kwake ila akamjibu kwamba atamfikiria kwenye suala hilo.

Picha ya pamoja Billnass na Nandy

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital msanii huyo ameeleza kuwa  "Tutawapokea watoto wowote ambao Mungu atakuwa ametubariki ila Billnass yeye anapenda kuwa na watoto 6, tutamfikiria" amesema Nandy 

Aidha Nandy amesema pete ambayo aliyovalishwa na mpenzi wake huyo mwaka jana imepotea wakati anafanya shughuli za Kampeni, hivyo tukio hilo litarudiwa tena.

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.