Tuesday , 18th Nov , 2014

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini Tanzania imewataka watanzania kushiriki katika kuboresha mazingira ya upatikanaji wa elimu nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mabweni .

Naibu waziri elimu Mhe. Jennister Mhagama.

Akiongea jijini Dar es salaam Naibu waziri elimu Mhe. Jennister Mhagama wakati akiwatunuku vyeti watu na mashirika mbalimbali walioshiriki kuchangia elimu kupitia mfuko wa elimu wa mamlaka ya elimu Tanzania (TEA) katika kuhakikisha wanafunzi nchini wanasoma katika mazingira salama na rafiki kielimu.

Bi. Jennister ameongeza kuwa ushirikiano baina ya wananchi na Sekta ya Elimu katika kuchangia maendeleo ya Elimu kutaboresha sekta hiyo kwa kiwango kikibwa nchini Tanzania kuliko kila kitu kuiachia serikali kufanya.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa chuo Kikuu cha Ardhi ARU Prof. Idrissa Mshoro amesema mpango huo wa kuchangia kuboresha mazingira ya upatikanaji wa elimu kwa wasichana umeongeza kiwango cha wasichana wanaojiunga na chuo hicho kutoa Asilimia 19 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 38 hivi sasa