Monday , 1st Feb , 2021

Ugonjwa usio wa kawaida umekatisha safari ya masomo ya watoto wawili wa familia moja baada ya kuwasababishia ulemavu wa kudumu.

Mkuu wa wilaya ya Misenyi Kanali Denice Mwila

Watoto hao ni Jovinus Rwiza na Prudence Rwizaa, wakazi wa kijiji cha Ishunju, wilayani Missenyi mkoani Kagera amabo wamepoteza tumaini la kutimiza ndoto zao za kimasomo.

Akizungumza na EATV mama mzazi wa watoto hao Jeneroza Tryphon amesema kuwa watoto wake walizaliwa wazima lakini walipofikisha umri wa miaka tisa walipatwa na ugonjwa wa mifupa ya mikono, miguu na mgongo kupinda na mwili kuishiwa nguvu, hali iliyowafanya washindwe kuendelea na masomo.

Baadhi ya majirani waliozungumzia ugonjwa huo wamesema wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha watoto hao wanatibiwa lakini jitihada zao zimegonga mwamba kutokana na tatizo linalowasumbua kuonekana kuwa kubwa.

Aidha kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo DC kanali Denice Mwila amedai kuwa watoto hao wameingizwa katika mpango wa kunusuru kaya maskini (Tasaf) lakini bado wanapaswa kupatiwa msaada zaidi wa kimatibabu.