Tuesday , 15th Dec , 2020

Chama cha waigizaji Dar Es Salaam Tanzania, kimetangaza kifo cha msanii maarufu wa filamu Mzee Jengua ambaye amefariki dunia siku ya leo Disemba 15 majira ya asubuhi nyumbani kwa mtoto wake Mkuranga.

Picha ya marehemu Mzee Jengua

Aidha taarifa hizo zimethibitishwa na mke wake na taarifa kuhusu mipango ya mazishi itafanyika hukohuko kwa mwanaye Mkuranga kisha utazikwa siku ya leo Disemba 16, saa 4 Asubuhi katika makaburi yaliyopo Mburahati, Dar Es Salaam.

EATV & EA Radio Digital, imepiga stori na msanii wa filamu Steve Nyerere na amemzingumzia Mzee Jengua ambaye waliwahi kufanya filamu moja ya Mke mwema.

"Taarifa tumezipokea tunasubiria vikao vya familia yake ili tukampumzishe mzee wetu, unapotamka Jengua unakuwa umetaja jina kubwa sana kwenye soko la filamu hapa nchini Tanzania, alikuwa mcheshi sana,ukimuangalia hachoshi na ana vituko vingi, mimi nimecheza naye filamu moja ya Mke mwema na alikuwa kama baba mkwe wangu" ameeleza Steve Nyerere

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.