Friday , 11th Dec , 2020

Ligi kuu soka Tanzania bara raundi ya 15, itaanza kutimua vumbi hii leo Desemba 11, 2020, kwa mchezo mmoja utakaopigwa mkoani Morogoro, ambapo Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa KMC mchezo utakaochezwa uwanja wa Jamhuri Morogoro, Saa 10:00 Jioni.

Mtibwa Sugar hawajawahi kushinda mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ya Dar es salaam katika michezo 4

Wenyeji Mtibwa Sugar hawajawahi kushinda mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ya Dar es salaam katika michezo 4. Mtibwa wamefungwa mara 3 na wamepata sare mchezo 1. Na msimu uliopita KMC walishinda michezo yote 2, ukiwemo ushindi wa bao 1-0 katika dimba la Jamhuri ambapo mchezo wa jioni ya leo utachezwa.

Timu hizi zinatofautiana kwa alama 5 kwenye msimamo wa ligi, KMC wapo juu ya Mtibwa Sugar, kwa tofauti ya alama hizo wakiwa na alama 21 wapo nafasi ya 5, wakati Mtibwa Sugar wapo nafasi ya 14 wakiwa na alama 16.

Wenyeji wa mchezo huu wakatamiwa wa Manungu wameshinda mchezo 1 kwenye michezo 6 ya mwisho ya ligi, wakitoka sare michezo 2 na wamefungwa michezo 3. Wakati KMC wamefungwa mchezo 1 kwenye michezo 6 ya mwisho, wameshinda michezo 3 na wamesare mchezo 1.