Rais Magufuli
''Hapo nataka kusema ukweli tuelewane hili la matumizi mabaya. Unakuta mkurugenzi ananunua gari la milioni 400 fedha tumehangaika nazo kuzipata wananchi, watoto wanachangishwa unakuta madawa hayatoshi. Nataka kazi yako ya kwanza kwenda kumsimamisha mkurugenzi wa Geita ndio kazi yako ya kwanza ukaanze nayo'' - Dkt. Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amemtaka Waziri Jafo kusimamia vizuri matumizi ya pesa kwenye Wizara hiyo kwasababu ndio changamoto kubwa iliyoonekana na ilimfanya afikirie sana kumrejesha kwenye nafasi yake.
“Tamisemi kuna matumizi mabaya ya fedha Jafo (Suleiman- Waziri wa Tamisemi) umefanya vizuri sana lakini kwenye kudhibiti fedha bado, nimefikiria sana kukurudisha au kutokukurudisha'', amesema Magufuli.
Baraza la Mawaziri limeapishwa leo Desemba 9, 2020, ambapo jumla ya Mawaziri 22 na Manaibu Mawaziri 23 wameapishwa katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Dodoma.

