Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Akizungumza mwishoni mwa wiki Jijini Arusha, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu katika Mkutano wa Kimataifa wa kikanda , ulioshirikisha nchi zaidi ya 9 ulimwenguni, ambao uliokuwa ukijadili mikakati na mbinu ya kukabiliana na mauaji ya tembo na wanyama wengine, katika hifadhi mbambali kwenye nchi hizo, amesema endapo wataondoa sheria zenye makosa na kuziboresha majangili wataogopa.
Nyalandu amesema haridhishwi na Sheria za sasa hivi kwani adhabu zinazotolewa kwa watuhumiwa wa ujangili ni ndogo, ila Wizara wanatarajia kupitia Sheria zote zinazohusu makosa dhidi ya wanayamapori, kwa lengo la kuweza kuangalia namna ya kuongeza adhabu.
Amesema hadi hivi sasa silaha zaidi ya 3,000 zinazotumika katika vitendo vya ujangili, ikiwemo sihala za kivita kama vile AK 47 na Gobore,zimeweza kukamatwa na kwa kipindi cha Mwaka 2013, watuhumiwa 1816 walikamatwa na kesi zao zinaendelea katika Mahakama mbalimbali hapa nchini.