
Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa MSD Laurean Bwanakunu.
Mwendesha mashtaka huyo ameeleza hayo leo Oktoba, 19,2020, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Richard Kabate,na kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 4,mwaka huu.
Miongoni mwa mashitaka yanayowakabili washtakiwa ni kati ya tarehe 1 Julai, 2016 na 30, June, 2019 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, kwa makusudi washtakiwa waliongoza genge la uhalifu.
Shtaka la pili ni kuisababishia hasara MSD, tukio wanalodaiwa kulitenda kati ya Julai mosi, 2016 na tarehe 30 June, 2019, katika eneo la MSD lililopo Keko, washtakiwa waliisababishia MSD hasara ya shilingi bilioni 3.8.
Pia, Bwanakunu, anadaiwa kati ya tarehe 1 Julai, 2016 na 30 Juni, 2019 katika Ofisi za MSD zilizopo Keko, kwa makusudi alikiuka sheria ya umma kwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kuwaongezea nyongeza ya mishahara na posho wafanyakazi wa MSD, bila kibali cha Katibu Mkuu Utumishi, na hivyo kuisababishia hasara mamlaka hiyo kiasi cha shilingi bilioni 3.
Shtaka la nne ni kuisababishia hasara ya shilingi 85 milioni mamlaka, shtaka linalowakabili washtakiwa wote, huku katika shtaka lingine wakituhumiwa kutakatisha fedha kiasi cha shilingi bilioni 1.6.