Friday , 9th Oct , 2020

Mshambuliaji chipukizi wa Borussia Dortmund, Erling Haaland atakosekana kwenye fainali za mataifa ya Ulaya zitakazochezwa kwenye mataifa mbalimbali mwakani baada ya timu yake ya Taifa ya Norway kufungwa na Serbia bao 2-1.

Erling Haaland akiwa na timu yaTaifa ya Norway

Athari ya kukosekana kwenye michuno hii, ni kupunguza wigo wake wa kutwaa tuzo mbalimbali za soka katika ngazi za Dunia, ikiwemo ya mchezaji bora wa Ulaya, tuzo ya mchezaji bora wa dunia (Ballon d'or )na ile tuzo mchezaji bora wa kiume wa FIFA.

Haaland amekuwa na takwimu bora ambapo tangu aanze kucheza soka la kulipwa mwaka 2018 akiwa na klabu ya Molde, aliwafungia magoli 14 katika michezo 39, vilevile aliifungia Red Bull Salzburg magoli 17 kwenye mechi 18.

Akiwa na Borusia Dortmund ameishaifungia mabao 17 katika mechi 18 ngazi ya klabu, huku akiifungia timu yake ya taifa bao 3 katika michezo 5.