Thursday , 8th Oct , 2020

Jeshi la Polisi mkoa wa Mjini Magharibi visiwani Zanzibar, linawashikilia watu wawili akiwemo mwanafunzi wa kidato cha kwanza kwa tuhuma za kumbaka na kumuingilia kinyume na maumbile mtoto wa darasa la nne katika shule ya msingi Taifa.

Pingu

Katika taarifa yake Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa Mjini Magharibi Awadhi Juma Haji amesema kijana anaetambulika kwa jina la Shaaza Mohammed Abasi, mwanamme mwenye umri wa miaka 14 alimuingilia muhanga huyo kwa siku mbili tofauti.

Aidha, Jeshi la Polisi pia linamshikilia mwanamme mwingine Dillo Thobias Shilande mwenye umri wa miaka 30 kwa tuhuma za kumrubuni muhangaa huyo huyo na kumuingilia kinyume na maumbile watuhumiwa wote wawili ni wakaazi wa Mwera mkoa wa Mjini Magharibi wilaya ya Magharibi A.

Wakati huo huo Kamanda Awadhi amesema kijana aliejuilikana kwa jina la Anuar Juma Seif, mwenye umri wa miaka 16 amefariki dunia baada ya kuzama baharini maeneo ya Mazizini mkoa Mjini Magharibi wakati akiogelea na wenzake.