Thursday , 8th Oct , 2020

Nahodha msaidizi wa Taifa Stars, John Bocco atakosekana katika kikosi kitakachoikabili Burundi, Oktoba 11 mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ambao ni mtanange wa kimataifa ya kirafiki.

Nahodha msaidizi wa Taifa Stars, John Bocco (Pichani) katika moja ya mchezo wa Stars.

Kwa mujibu wa Kocha mkuu wa timu hiyo, Etienne Ndairagije amesema Bocco anaendelea na matibabu kwakuwa bado hajawa timamu kiafya na wameamua kumpa nafasi ya kuendelea kupatiwa matibabu.

Aidha Etienne amesema wachezaji wote walishajiunga na kambi ya Stars kasoro Himid Mao Mkami ambaye alikua bado hajawasili kutokea Misri.

Taifa Stars itashuka katika dimba la Benjamin Mkapa siku ya Jumapili kucheza na Burundi (Intamba Murugamba ) mtanange ambao matokeo yake yanaweza kuipandisha nchi katika viwango vya ubora vya Shirikisho la soka Duniani( FIFA)