Thursday , 8th Oct , 2020

Watafiti wa elimu kwenye Demokrasia Tanzania, (REDET),wamesema watashiriki kikamilifu katika kuhakikisha uchaguzi Mkuu unakuwa wa haki na uwazi ili kila mtu ama chama kiweze kupata haki inayostahili.

Mwenyekiti wa REDET, Prof. Rwekeza Mukandala (Kulia) akizungumza na Vyombo vya habari

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa REDET, Prof. Rwekeza Mukandala, leo katika kikao cha Waandishi wa habari kilichofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaaam ambapo amesema katika kutekeleza haki katika Uchaguzi Mkuu Tanzania Bara na Visiwani wataangalia na kupima uhalali,usawa na haki kwenye uchaguzi huo.

Aidha Prof.Mkandala amesema watahakikisha wanaangalia namna ya vyombo vya utawala hasa NEC na ZEC zinafanya kazi zake kama kweli vinatenda haki kwa wahusika.

Aidha amesema kuwa waangalizi hao watapima namna ambavyo vyombo vya habari, vitakavyo wajibika katika kuwapa usawa wagombea na wapiga kura lakini pia matumizi ya mali za Umma.