
Meneja wa kituo cha mabasi cha Ubungo, Mahela Nkhama Chilosa.
Akiongea na EATV, Chilosa amesema awali serikali ilishasema kwamba mwisho wa matumizi ya kituo cha mabasi Ubungo ni mwezi wa kumi lakini kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya vitu ndio sababu inayofanya kituo hicho kisihame kwa wakati.
''Hapa kwa sasa tupo lakini sidhani kama katika kipindi cha mwezi mmoja ujao tutakuwepo na nafikiri hata hizi kampeni nazo zimechangia maana viongozi wengi wapo huko'', amesema Chilosa.
Ameongeza, hata baadhi ya mabasi yameshaanza kuondoka ndani ya kituo na kutumia maeneo yao ya kuegesha mabasi hayo kama ndio kituo cha kupanda na kushusha abiria.