
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde.
Akizungumza na vyombo vya habari Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika ikiwemo kusambazwa kwa karatasi za mitihani, fomu maalum za ‘OMR’ za kujibia mitihani na nyaraka zote muhimu zinazohusika katika mtihani huo katika Halmashauri na Manispaa zote nchini.
“Baraza linatoa wito kwa wasimamizi wote walioteuliwa, kufanya kazi yao kwa uadilifu wa hali ya juu na wahakikishe wanalinda haki ya watahiniwa wenye mahitaji maalum” amesema Dkt. Msonde.
Ameongeza kuwa, Baraza linawataka wamiliki wa Shule kutambua kuwa shule zao ni vituo maalum vya mitihani na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani.