
Rais wa TFF Wallace Karia(Wa pili kutoka kushoto), akiwa na Makamu wake Athumani Nyamlani( Wa pili kutoka kulia), Katibu Wilfred Kidao(Wa kwanza kutoka kushoto) na Mkuu wa Masoko Michael Wambura (Wa kwanza kulia) katika hafla ya kusaini mkataba na SBL.
Akiongea mara baada ya kusaini kandarasi hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam, Raisi Karia amesema kandarasi hiyo ni ya miaka mitatu na wameingia na wadhamini wao walewale waliomaliza muda wao kampuni ya Serengeti Breweries.
“Fedha zilizotolewa kwa ajili ya udhamini huo zitatumika kama ilivyokusudiwa katika kufanikisha uendeshaji ya timu na hivyo kupata matokeo mazuri katika michezo yake” amesema Karia
Taifa Stars ipo kambini chini ya Kocha Mkuu Etienne Ndayiragije kujiandaa na mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Burundi unaotarajiwa kupigwa katika uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar Es Salaam mnamo Oktoba 11 mwaka huu.
Ushindi wa Taifa Stars katika mchezo huu ni wa maana sana kwani ni mchezo unaotambuliwa na kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani FIFA hivyo unaweza kuathiri daraja la taifa husika katika viwango vya ubora wa dunia
Timu ya taifa ya Burundi itaongozwa na nyota wake Saido Berahino anayekipiga nchini Ubelgiji kwa mkopo katika klabu ya Royal Charleroi Sporting Club na aliwahi kuichezea klabu ya Ligi Kuu nchini Uingereza West Bromwich Albion msimu wa 2010-17
Wakati Taifa Stars itaongozwa na nahodha Mbwana Ally Samatta anayekuputa katika klabu ya Fenerbahce kwa mkopo akitokea Aston Villa ya Uingereza aliyoichezea kwa nusu msimu 2019-20.