Tuesday , 6th Oct , 2020

Nyota namba moja wa tenisi Duniani kwa wanaume Novak Djokovic, ametinga robo fainali ya michuano ya wazi ya Ufaransa baada ya kumshinda Karen Khachanov raia wa Urusi kwa 6-4 6-3 6-3.

Novak Djokovic

Djokovic ambaye alishinda taji la Ufaransa mnamo 2016, analenga kuwa mtu wa kwanza katika enzi za uwazi kushinda kila Grand Slams mara mbili.

Raia huyo wa Serbia ameweka rekodi mpya katika michuano hiyo kwa kufuzu hatua ya robo fainali kwa mwaka wa  11 mfululizo.

Nyota namba moja wa tenisi Duniani kwa wanaume Novak Djokovic

Katika hatua hiyo ya robo fainali Djokovic, atakabiliana na  Pablo Carreno Busta raia wa Hispania.

Katika mchezo mwingine Stefanos Tsitsipas wa Ugiriki, alifika robo fainali yake ya kwanza kwa ushindi dhidi ya  Grigor Dimitrov raia wa Bulgaria.