Monday , 5th Oct , 2020

Mshambuliaji wa Uholanzi, Memphis Depay atajiunga na Barcelona muda wowote kabla ya dirisha la usajili Ulaya kufungwa leo.

Memphis Depay akiwa kwenye mechi za Lyon

Memphis ambaye anaichezea Lyon ya Ufaransa, amekuwa akihusishwa na Barcelona muda mrefu tangu kocha Ronald Koeman kuchukua mikoba katika timu hiyo.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa michezo wa Lyon, Juninho Pernambucano amesema“Pande mbili kati ya mchezaji na Barcelona zimekubaliana kila kitu, kilichobaki ni makubaliano ya klabu na klabu, tunaamini watafanya haraka kwa kuwa dirisha la usajili linafungwa rasmi leo ''.

Ikiwa uhamisho huu utafanikiwa, Depay anayetajwa kwenda kuziba pengo la Luis Suarez aliyetimukia katika klabu ya Atletico Madrid.

JE DEPAY KUZIBA PENGO L A SUAREZ?

Depay alimaliza msimu wa ligi kuu nchini Ufaransa akiwa na magoli 15 aliyofunga katika michezo 22 aliyocheza.Alikua na mchango mkubwa kwa Lyon ambayo ilicheza nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Takwimu zake zinavutia kwani tangu ajiunge na miamba hiyo ya Ufaransa mwaka 2017 akitokea Manchestesr United, amecheza jumla ya michezo 144 na amefunga magoli 58.

Kwa takwimu hizo ina ashiria kwamba anauwezo mzuri wa kufunga kama ilivyokua kwa Luis Suarez ambaye alifunga mabao 198 katika michezo 283 alipokua na Barcelona.

JE BARCELONA INABAHATI NA WAHOLANZI?

Depay atakuwa mchezaji wa 20 raia wa Uholanzi kuitumikia Barcelona katika historia ya klabu hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1899.

Baadhi yao ni Johan Cruff,Ronald Koeman ambaye ni ( kocha wa sasa wa Barcelona)Patrick Kluivert, Marc Overmars,Edgar Davis na mapacha wawili Frank na Ronald De Boer.