
Jimmy Butler
Jimmy Butler wa Heat, alipata triple double baada ya kumaliza na pointi 40, assists 13 na rebounds 11.
Butler sasa ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu kufunga pointi 40 na triple-double kwenye fainali za NBA. Wachezaji wengine ambao wamewahi kufanya hivyo ni LeBron James na Jerry West ambaye kwasasa ni miongoni mwa maofisa wa NBA.
Jimmy Butler kwenye mechi dhidi ya Lakers
Nyota wa Lakers LeBron James alimaliza mchezo huo akiwa na pointi 25, assists 8 na rebounds 10.
Ushindi huo wa Miami Heat umefanya matokeo kuwa 2-1 Lakers wakiongoza series.
Mchezo wa nne wa fainali hizo utapigwa kesho Jumanne Oktoba 6, 2020.