Friday , 2nd Oct , 2020

Mkongwe wa Bongo Fleva Dully Sykes amesema alipata umaarufu kabla haijaingia mitandao  ya kijamii ambayo kwa sasa ndiyo chachu ya kusaidia kuongeza umaarufu kwa wasanii wengi kitu ambacho hakikuwepo kwa upande wake ili kukuza kipaji chake.

Msanii wa BongoFleva Dully Sykes

Akizungumza  hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Dully Sykes  ameeleza kuwa hakuna kitu kinachoweza kumpa mtu umaarufu tofauti na kuchapa kazi.

"Kuwa tajiri au masikini ni majaliwa ya Mungu, mimi nilipata umaarufu kabla ya Facebook, WhatsApp, Instagram na Twitter, kazi ndiyo inambeba msanii ili kufikia mafanikio, hakuna mzembe anayefanikiwa hata ukitumia mitandao yote kama huna juhudi haina maana hata meneja huwa wanaangalia msanii anajitahidi vipi" amesema Dully Sykes 

Aidha msanii huyo ameongeza kuwa "Kuna watu wameumbwa kusaidia watu hata wakitendwa mimi nasaidia wala sisubiri fadhila kutoka kwa mtu, nasaidia mtu nikamaliza nafanya mambo yangu na yeye afanye yake"