
Mgombea urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu.
Lissu kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa ataendelea na ratiba zake ikiwemo kikao cha mabalozi kinachofanyika leo.
"Wito wa polisi sio barua ya kirafiki ni amri kisheria, wito huo unatakiwa kueleza kosa la mtuhumiwa barua hii haielezi kosa ninaloitiwa na imepelekwa kwa Mwenyekiti wa chama, huu sio wito wa polisi kwa mujibu wa sheria, nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi kesho" ameandika Lissu kupitia kaunti yake ya Twitter.
Kwa mujibu ya barua iliyotumwa kwa Mwenyekiti wake wa Chama, Freeman Mbowe, Lissu anatakiwa kuripoti polisi leo 02/10/2020 kwa ajili ya mahojiano kufuatia kauli na matamshi yake ambayo amekuwa akiyatoa kwenye mikutano yake ya kampeni dhidi ya maafisa wa polisi.