
Thiago katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Chelsea aliweka rekodi ya kupiga pasi 75 zilizokamilika ambazo zilikuwa nyingi kuliko mchezaji yoyote wa Chelsea licha ya kucheza dakika 45 tu
Kiungo huyo raia wa Hispania amejiunnga na Liverpool mwezi huu na alicheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Chelsea wiki iliyopita, lakini hakuwa sehemu ya kikosi kilichocheza mchezo wa ligi dhidi ya Arsenal jana Usiku mchezo amabao Liverpool walishinda kwa mabao 3-1.
Baada ya mchezo huo Jurgen Klopp alipoulizwa kwa nini Thiago hakuwa sehemu ya kikosi alisema
‘Baada ya mapumziko ya kimataifa atakuwa sawa, kwa hakika, hivyo ndivyo ilivyo kwa sasa hakuwa sawa kucheza mchezo wa leo”
Michezo miwili atakayokosa Thiago ni mchezo dhidi ya Arsenal utakao chezwa siku ya Alhamisi mchezo wa raundi ya nne wa kombe la ligi Carabao CUP mchezo mwingine ni wa ligi kuu dhidi ya Astoni Villa utakao chezwa Jumapili.
Alcantara anatarajiwa kurejea kwenye mchezo wa dabi ya Jiji la Liverpool (Merseyside Derby ) mchezo dhidi ya Everton utakao chezwa Octoba 17 katika dimba la Goodson Park.
Na bado inasubiliwa kama kocha wa timu ya Taifa ya Hispania Luis Enrique atamtaja Thiago kwenye kikosi chake kitakacho cheza michezo mitatu mwezi huu dhidi ya Ureno, Switzerland and Ukraine.