Tuesday , 29th Sep , 2020

Shilole kumuandika Uchebe ndiyo linaweza likawa swali kubwa kwa watu wengi baada ya msanii huyo kutangaza kufikiria kuachia kitabu chake ambacho kitaacha alama na kitakachohusu mfumo mzima wa maisha kwa ujumla.

Uchebe na Shilole enzi zao walipokuwa kwenye ndoa

Shilole amehabarisha hilo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ambapo ameandika kuwa

"Nafikiria kuandika kitabu, nafikiria kuacha alama, nafikiria kuelezea mapito na magumu yaliyonijenga leo hii kuwa Shishi,  haikuwa rahisi hata kidogo lakini pia hakuna gumu unapoamua kutokukata tamaa, kuweka juhudi, kumumuweka Mungu mbele na kuzikimbiza ndoto zako"

Shilole ni mmoja wa watu maarufu na wenye ushawishi kwa wanawake wengi kwa sasa kuanzia kazi na biashara zake kutokana na mafanikio aliyoyapata na vitu ambavyo amepitia kama kubakwa, kupata watoto akiwa na umri mdogo, kubezwa kwenye filamu na muziki, na kubwa zaidi kupigwa na aliyekuwa mume wake Uchebe.