
Msanii wa BongoFleva Rhino King
Akifunguka kupitia eNewz ya East Africa TV Rhino King amesema “Kupaka rangi katika kucha zangu kwanza familia yangu hawajaliongelea hilo inakuwaje watanzania kuliongelea, nilianza kupaka rangi kabla sijakuwa mbele ya vyombo vya habari, sio kitu cha kuwapa watu attention, style ya kupaka rangi kucha kwangu ni ya kipekee"
“Mtoto wakiume kupaka rangi kwenye kucha ni sawa tu na wa kike kupaka rangi watanzania wayaache tu maisha yangu mengine hata mwanzo nilikuwa na dread kichwa kizima sasahivi nina dread upande mmoja maisha yanabadilika watu wajifunze kuwa kila mtu na maisha yake” ameongeza