
Winga wa Watford Ismaila Sarr akiwa kwenye majukumu ya timu yake
Maamuzi haya ya Solskjaer yanachangiwa na muda mchache uliyobaki kabla ya dirisha la usajili kufungwa rasmi 4/10/2020, huku Dortimund wakihitaji fedha nyingi zaidi ya paundi milioni 108 ili kumruhusu Sancho kujiunga na United.
Sarr raia wa Senegal amewashawishi United kama chaguo la pili kutokana na kuwa na msimu mzuri uliopita pamoja na msimu kuathirika na janga la Corona, ambapo alifunga magoli 6 katika michezo 30 aliyocheza,
NI MBADALA SAHIHI WA SANCHO?
Kuna vitu wanafanana, na kuna vitu wanatofautiana,wanafanana kwenye kasi yao na uwezo mzuri wa kupiga krosi nzuri kwa wakati, lakini wanatofautiana kwenye uwezo wa kufunga, Sancho anauwezo zaidi wa kufunga na kutoa pasi msaada, kwa msimu uliopita alifunga goli 17 na kutoa pasi msaada 17 katika mechi 32 alizocheza