Friday , 31st Oct , 2014

Wakili wa Vilabu shiriki vya Ligi kuu Tanzania Bara,Damas Ndumbalo amesema Shirikisho la soka nchini TFF halina mamlaka dhidi yake ya kumshimamisha kuvitetea Vilabu shiriki vya Ligi Kuu.

Wakili Damas Ndumbalo

Akizungumza jijini Dar es salaam, Ndambaro amesema kama TFF waliona anakosa,malalamiko wangeyapeleka kwa Jaji mkuu au kamati ya maadili ya mawakili na kabla ya kufikia makubaliano ya kuvitetea vilabu hivyo juu ya TFF kukata asilimia Tano katika mapato ya mechi, alivitaka vilabu hivyo kutiliana saini ambapo vilabu vyote vilikubali isipo kuwa timu ya Stand United ya mjini Shinyanga.

Ndumbaro amesema TFF ilitoa hukumu bila kumsikiliza kwa kuwa alitoa taarifa ya safari yake ya kikazi na kuomba TFF waahirishe kesi lakini hawakufanya hivyo, hivyo Oktoba 21 aliamua kukata rufaa katika kamati ya rufaa ya Nidhamu ambayo hadi sasa hajaona dalili za kusikilizwa kwa rufaa hiyo.