Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene.
Akizungumza hii leo Septemba 23,2020, katika mkutano wa maandalizi ya uandishi wa kitabu kuhusu miaka 60 ya kuhifadhi wakimbizi nchini Tanzania uliofanyika katika mkoa wa Arusha amesema Tanzania haijawahi kufanya operesheni yoyote katika mpaka wa Uganda kwa ajili ya kuwafukuza wakimbizi.
“Nchi yetu imekuwa ikipokea waomba hifadhi na kuhifadhi wakimbizi hata kabla ya uhuru, hata hivyo historia kubwa, ndefu na yenye thamani inaanza na Rais wa Awamu ya Kwanza na Baba wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu J.K. Nyerere” amesema Simbachawene.
"Tanzania inahistoria kubwa ya kuhifadhi na kuwatunza wakimbizi,haijawahi kufanya operesheni yoyote katika mpaka wa Uganda kwa ajili ya kuwarejesha wakimbizi"ameongeza.
Aidha Simbachawene amesema kuwa baada ya kupata taarifa hizo aliwauliza serikali ya mkoa wa Kagera ambao walikataa kuwepo kwa kitendo hicho.