Aliyewahi kuwa RPC Arusha, ACP Jonathan Shana
Akizungumza na EATV&EA Radio Digital mapema leo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano hospitalini hapo Aminiel Aligaesha amethibitisha hilo na kusema kuwa marehemu alikaa hospitalini hapo kwa siku 21 na kati ya hizo alikaa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU), kwa siku tatu.
"Jonathan Shana, Mstaafu RPC Mkoa wa Arusha amefariki usiku wa kuamkia leo Septemba 16, 2020, amelazwa hapa Muhimbili kwa siku 21, na kati ya siku hizo ICU amekaa siku 3", amesema Aligaesha.
Ikumbukwe kuwa Juni 24 mwaka huu, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, alimhamisha ACP Shana kutoka kuwa RPC na kwenda kuwa afisa mnadhimu shule ya Polisi Moshi.