Wednesday , 29th Oct , 2014

Mrembo Leah Kalanguka ambaye amefanikiwa kutwaa taji la Miss Uganda 2014, amefunguka kufuatia mjadala mkubwa unaoendelea mtandaoni juu ya muonekano wake, na amesema kuwa kila mtu ana haki kusema anachojisikia, na hawezi kuacha mitandao kumshusha.

Leah Kalanguka, Miss Uganda 2014

Leah amesema kuwa, Urembo si namna ya muonekano wa nje bali ni kilicho ndani ya mtu na kile anachoweza kuonesha dunia, huku akikazia kuwa yupo tayari kuiwakilisha nchi yake katika mashindano ya Miss World mwezi Desemba mwaka huu.

Kufuatia mrembo huyu kukosolewa sana mtandaoni, watu maarufu pia kama Bobi Wine na Anne Kansiime wamemtetea mrembo huyu na kutaka watu kuacha kumkosoa mrembo huyu bila kufahamu ni kwa namna gani amepambana kushinda nafasi hii.