Masinga amesema japo baadhi ya wachezaji katika timu hiyo ni majeruhi lakini anategemea mwishoni mwa wiki hii wataanza mazoezi ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa ajili ya mashindano hayo yenye ushindani mkubwa hapa nchini yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 12 hadi 16 mwaka huu katika Uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam.
Msinga amesema michuano hiyo inayotarajiwa kushirikisha nchi za Kenya, Uganda Rwanda na wenyeji Tanzania ina ushindani mkubwa kutokana na vilabu kutoka nje ya nchi kuchukua ushindi katika michuano hiyo, lakini kwa mwaka huu wamejipanga kwa ajili ya kubakiza kombe nchini.