
Meneja wa ACT Wazalendo Emmanuel Lazaro akizungumza na waandishi wa habari
Katika mkutano na waandishi wa habari meneja kampeni wa Chama Hicho Emmanuel Lazaro amesema takribani asilimia 74 za wagombea wao wamepata nafasi za uteuzi kwenye majimbo mbalimbali huku akieleza kuwa Baadhi ya wasimamizi wa Uchaguzi kuwa changamoto.
Bw Lazaro amesisitiza kuwa wanatarajia kutoa ratiba ya kampeni kuanzia kesho pamoja na kuzindua ilani ya Uchaguzi siku ya Jumapili ya Agosti 30.
Chama Cha ACT Wazalendo ni Kati ya vyama 15 ambavyo Tume ya Taifa ya uchaguzi imevipitisha kusimamisha mgombea kwa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bernard Membe