Kufuatia agizo la Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini LATRA kuwataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kuanza kutoa huduma ya tiketi kwa njia ya kimtandao suala Hilo limeonesha kuleta mkanganyiko mkubwa kwa wamiliki wa vyombo Hali ambayo imetufanya EATV kuwatafuta Chama Cha Wamiliki wa vyombo vya usafiri kujua Nini hasa kinacholeta utata Hadi kuiomba Wizara yenye dhamana kuingilia mchakato huo ili kuweka mizania sawa na kuondoa sintofahamu hiyo.
"Ni vyema Sasa waziri mwenye Dhamana ya uchukuzi akaingilia Kati ili Mfumo huu utazamwe upya ili kuangalia mrundikano wa tozo zitakazotokana na Mfumo huu kuliko kupelekewa Taarifa na watendaji kutoka kwenye hizi Mamlaka pekee "Mustafa Mwalongo Mkurugenzi wa Habari TABOA.
Amesema Teknolojia ni jambo zuri lakini wamiliki wengi wa vyombo hawana Elimu hiyo hivyo ni vyema elimu ingewekezwa zaidi ili kuondoa maswali mengi ambayo watu wekuwa wakijiuliza kuhusu mrundikano wa tozo uliopo kwa washiriki wa Mfumo huo.
"Huu Mfumo bado unashida kubwa unajua wamiliki wengi wa mabus hizi za Kimtandao Elimu hawana hivyo ni vyema LATRA ikajikita kutoa elimu kwa wamiliki kuliko kuendelea kuvutana" alisema Mustafa Mwalongo Mkurugenzi wa Habari TABOA.
Mfumo huo wa tiketi kwa njia ya kimtandao ulipashwa kuanza kufanya kazi tangu Tarehe moja mwezi August 2020.