Tuesday , 28th Jul , 2020

Aliyekuwa Askofu Mkuu Jimbo la Dar es Salaam Askofu Mstaafu Polycarp Pengo na Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania leo wameshiriki katika ibada ya misa ya kuuaga mwili wa aliyekuwa rais wa awamu ya tatu Tanzania hayati Benjamin William Mkapa katika kanisa la Immaculata Upanga.

Mjane wa Hayati Mkapa mama Anna Mkapa akisaidiwa kuelekea eneo la Kuaga mwili wa marehemu mume wake.

Aliyekuwa Askofu Mkuu Jimbo la Dar es Salaam Askofu Mstaafu Polycarp Pengo na Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania leo wameshiriki katika ibada ya misa ya kuuaga mwili wa aliyekuwa rais wa awamu ya tatu Tanzania  hayati Benjamin William Mkapa katika kanisa la Immaculata Upanga alipokuwa anasali Hayati Mpaka umauti ulipomfika.

Akizungumza baada ya misa hiyo Paroko wa Kanisa hilo Padri Casmir Kavishe amesema kuwa Marehemu Mkapa alikuwa mcha Mungu na mwaminifu ikiwemo kuhudhuria ibada na alipenda kujulikana kama mwanaparokia wa kawaida pasipo kuhusisha vyeo kulingana na hadhi yake.

“Sisi tutamkosa tunamuomba Mungu aweze kumpokea na tuliobaki tuweze kuyaishi yale mema aliyofanya Mpaka aliwahi kwenye ibadani ni msingi bora aliouweka kwa wanaparokia wote”alisema Padri Kavishe.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Yohana Mbatizaji aliyokuwa akishiriki na Msemaji wa familia William Erio amesema kuwa marehemu Mkapa ameshiriki katika ibada zote na kuwa ibada hiyo imefanyika kutokana na maagizo aliyotoa kuwa endapo akifariki ifanyike hapo kabla ya kuzikwa kijijini kwake Lupaso.

Baadia ya ibada ya misa hiyo kanisani hapo mwili wa hayati Mpaka ukapelekwa katika uwanja wa Uhuru kwa Heshima za mwisho zilizotanguliwa na maombi na dua kutoka kwa viongozi wa dini kusomwa wasifu na salamu za rambimrambi kutoka kwa wageni wa kimataifa na mabalozi.

Mwili wa Hayati Mkapa utasafirishwa leo kuelekea kijijini kwao Lupaso Wilayani Masasi Mkoani Mtwara kwa ajili ya maziko yatakayofanyika kesho tarehe 29/07/202.