Monday , 27th Jul , 2020

Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa Yanga SC Mwinyi Zahera ameonyesha kusikitishwa na kauli za kocha mkuu wa klabu hiyo Luc Eymael juu ya Shirikisho la soka nchini,Viongozi na Mashabiki wa wana Jangwani hao kwa kuwaita majina ya kibaguzi baada ya mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya

Kocha Mwinyi Zahera

Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa Yanga SC Mwinyi Zahera ameonyesha kusikitishwa na kauli za kocha mkuu wa klabu hiyo Luc Eymael juu ya Shirikisho la soka nchini,Viongozi na Mashabiki wa wana Jangwani hao kwa kuwaita majina ya kibaguzi baada ya mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Lipuli FC.

Akizungumza kwa njia ya simu Zahera amesema amesikitishwa sana na kauli za kocha huyo huku akisisitiza kuwa hafai kuwa kocha katika timu hiyo.

"Ni kitendo kibaya na cha kushangaza  sana katika msimu ambao umekuwa bora ni msimu huu kutoka,TFF Kufanya vizuri katika idara ya waamuzi lakini kocha kama huyu anasema mambo ambayo si mazuri kwa mashabiki hata uongozi"amesema Zahera.

Mapema uongozi wa klabu ya Yanga kupitia ukurasa wao wa instagram ulithibitisha kumfuta kazi kocha huyo k utokana na kauli zake na kusema utamwondoa nchini haraka iwezekanavyo.

Katika barua hiyo uongozi wa Yanga, pia umeiomba radhi Serikali, Shirikisho la soka Tanzania TFF, wanachama na mashabiki wa Yanga na Watanzania wote kutokana na kauli za kuudhi na kudhalilisha za  Luc Eymael.