Wednesday , 22nd Jul , 2020

Mama mzazi wa staa wa BongoFleva Alikiba, Abdukiba, Zabibu na Aboubakar Kiba, amesimulia jinsi mwanaye Alikiba alivyopotea kutoka Kariakoo hadi Vingunguti kisa ngoma za mdundiko.

Mama wa wasanii Alikiba na Abdukiba katikati akiwa na wanae

Akieleza tukio hilo kwenye mahojiano maalum na Msemaji Mkuu wa Wanawake Maryam Kitosi Mama Alikiba amesema kuwa,

"Alikiba alianza kucheza tangu akiwa na siku 7, katika ukuaji wake alikuwa akisikia muziki anaufuata, sasa siku hiyo ilipita ngoma ya kiluguru, Ali akaenda kuokotwa Vingunguti kutoka Kariakoo hadi Vingunguti, siku nyingine ikapita mdundiko akakutwa Kigogo jinsi mziki ulivyokuwa kwenye damu yake, nikaenda kuripoti Polisi mara nne ila nashukuru Mungu nilimpata jioni" amesema Mama Alikiba.

Zaidi tazama kwenye video hapa chini.