Meddie Kagere kinara wa mabao VPL
Kinara wa mabao katika ligi kuu Tanzania bara Meddie Kagere amesema kilichosababisha kufika katika nafasi hiyo ni kutokana na ushirikiano wake pamoja na wachezaji wanzake kwa kujituma na kuungana kwa pamoja katika kitafuta ushindi.
Aizungumza na Eatv baada ya mazoezi ya Simba SC katika viwanja vya Mo Simba Arena, Kagere amesema anashukuru Mungu kwa kumsaidia kuwa hapo pamoja wachezaji wenzake kumpa sapoti ya kutosha katika kuhakikisha anakuwa bora.
'' Mimi mpaka kila mechi nafunga nikutokana na ushirikiano ambao naupata kutoka kwa wachezaji wenzangu kwahiyo mafanikio yangu yanatokana na wao na siku zote wamekuwa wakiniambia wanaaniamini katika hilo'' amesema Kagere .
Aidha Kagere amesema uwepo wa mshambuliaji John Bocco unampa msada mkubwa kutokana na mchezaji huyo kuwa mzoefu na kiongozi ndani ya timu hiyo hali inayomfanya kujiamini na kushirikana naye kwa pamoja kuisaidia timu yake.
Meddie Kagere anaongoza orodha ya wafungaji wa ligi kuu akiwa na jumla ya mabao 22 akiwaacha Yusuph Mhilu wa Kagera Sugar mwenye mabao 13 pamoja na Waziri Junior mwenye mabao 12 huku akiwa na rekodi ya kuwa mfungaji bora katika msimu uliopita akiwa na mabao 23 akimshinda Salim Aiyee wa Mwadui fc aliyemaliza na mabao 20.


